• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaendeleza ubabe kwenye Marathon ya Chicago

    (GMT+08:00) 2014-10-15 15:17:12

    Kenya imeendelea kuonesha hadhi yake kuwa ni nchi isiyoshindikana duniani katika mbio ndefu baada ya wanariadha wake kutawala katika mbio za Marathoni za Chicago. Kwa upande wa wanawake Rose Jeptoo alinyakua ushindi huo kwa kutumia muda wa saa 2:24:35 huku wenzake wa kiume wakitawala kabisa mbio hizo na kuchukua medali katika nafasi zote tatu za juu. Katika kipengele cha wanaume Eliud Kipchoge alishinda kwa kutumia muda wa saa 2:4:11 na kuondoka nazo nyumbani dola 155, 000 kwa ushindi huo wa Marathon ya Chicago mwaka 2014 huku wenzake, Sammy Kitwara and Dickson Chumba wakichukua nafasi ya pili na tatu, wawili hawa walitumia muda wa 2:04:28 na 2:04:32, huku muethiopia Kenenisa Bekele akiwa wa nne kwa kutumia muda wa 2:05:51. Lakini ni Jeptoo, ambaye rikodi yake imeimarika na kuonekana ni vigumu kushindikana nchini Marekani baada ya kushinda marathoni mbili mfululizo yaani ya Chicago na Boston na kufuata nyayo za mkenya mwenzake Catherine Ndereba, ambaye alishinda kati ya mwaka 2000 and 2001.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako