• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yakaribisha makubaliano ya kibiashara kati ya EAC na EU.

    (GMT+08:00) 2014-10-16 12:22:05

    Shirikisho la wenye viwanda nchini Kenya limekaribisha kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara kati ya jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya. Mkurugenzi wa Shirikisho hilo Bibi Betty Maina amesema makubaliano hayo yaliyosainiwa mjini Brussels Ubelgiji yatasaidia kuokoa maelfu ya ajira ambazo zilikuwa kwenye hatari kutokana na kucheleweshwa kwa mazungumzo.

    Makubaliano hayo sasa yatawezesha Kenya kuendelea kuuza bidhaa bila ushuru kwenye soko la Ulaya. Iwapo makubaliano hayo yasingesainiwa asilimia 22% ya mauzo ya Kenya barani Ulaya yangeathiriwa, asilimia 9% kati ya hayo yakiwa ni mauzo ya maua.

    Umoaj wa Ulaya hununua asilimia 60% ya bidhaa kutoka Afrika Caribbean na Pasifiki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako