Algeria imekuwa nchi ya kwanza kufuzu michuano ya kombe la mataifa ya Afrika baada ya kuibanjua bila huruma Malawi kwa mabao 3-0. Goli la kwanza liliingizwa baada ya dakika moja ambapo Porto Yacine Brahimi alivurumisha pasi kali hadi kwenye wavu. Naye Riyad Mahrez ambaye anachezea ligi ya England katika klabu ya Leicester City akaongeza goli la pili huku la tatu likitiwa kimiani kwa kichwa na Slimani baada ya kupokea pasi kutoka kwa Mahrez na kuihakikishia nchi hiyo kucheza fainali hizo mwakani. Awali Ethiopia, licha ya kucheza dakika 30 za mwisho ikiwa na miamba 10 tu kiwanjani, iliweza kujinyanyua na kulipiza kisasi kwa kufungwa nyumbani kwao na kuwatandika Mali kwa mshangao magoli 3-2 huko Bamako. Matokeo hyo yanamaanisha kuwa Algeria ina pointi 12 na kuwa na uhakika kumaliza wakiwa katika nafasi mbili za juu, Mali imebaki kuwa ya pili licha ya kupoteza pointi 6, huku Malawi na Ethiopia zote zikiwa na pointi 3. Matokeo mengine katika mechi zilizochezwa jana jumatano ni kama ifuatavyo Cameroon 2-0 Sierra Leone, Togo 1-0 Uganda, Angola 4-0 Lesotho, Ghana 3-1 Guinea, Nigeria 3-1 Sudan, Zambia 3-0 Niger, Egypt 2-0 Botswana, Ivory Coast 3-4 DR Congo, Cape Verde 1-0 Msumbiji, Burkina Faso 1-1 Gabon, Mali 2-3 Ethiopia, South Africa 0-0 Congo, Tunisia 1-0 Senegal, na Algeria 3-0 Malawi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |