Mwanariadha wa Kenya Mary Keitany anataka kuongeza changamoto katika marathoni ya New York itakayofanyika Novemba 2, huku akiwa ana mpango wa kurejesha hadhi yake baada ya miaka miwili ya mapumziko. Mwanariadha huyo mwenye miaka 30 na mama wa watoto wawili, atakuwa anakimbia marathoni kwa mara kwanza na hizi zikiwa ni mbio zake za tatu katika miaka miwili atakaposhindana New York na kutegemea kuwa ataondokana na hofu na kumaliza mbio kama sio kushinda.Keitany amesema amekuwa akifanya mazoezi vizuri, na pia alipata nafasi ya kushindana na kujaribu mwili wake, hata hivyo amesisitiza kuwa hiki kitakuwa kikwazo kikubwa cha kwanza katika mpango wake wa kurejea tena kwenye marathoni. Kwa mara ya mwisho kushindana mbio ilikuwa ni katika Olimpiki ya London ambapo alikamata nafasi ya nne. Lakini kukamilisha umbali wa kilomita 42 itakuwa ni suali ambalo Keitany anaiachia miguu yake ilijibu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |