• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Binamu wa marehemu Reeva asema Pistorius anapaswa kupewa adhabu kali

    (GMT+08:00) 2014-10-17 10:12:04

    Binamu wa marehemu Reeva, Kim Martin ameiambia mahakama mjini Pretoria Afrika Kusini kuwa mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, anapaswa kupewa adhabu ya kutosha kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp. Martin alisema Pistorius, anapaswa kuadhibiwa vikali kwa makosa yake. Jaji, Thokozile Masipa, ameahirisha kesi hiyo hadi leo asubuhi. Upande wa utetezi, unasema kuwa Pistorius anapaswa kupewa kifungo cha nyumbani na kuhudumia jamii kwa kosa lake, pendekezo ambalo kiongozi wa mashitaka Garrie Nel ameelezea kushutushwa nalo.vUpande wa mashitaka unasisitiza Pistorius afungwe jela akisema kitendo chake kimesababisha huzuni na kadhia kubwa kwa familia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako