• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yanga, Coastal, Stand zaikana kamati ya TFF

    (GMT+08:00) 2014-10-17 10:12:26

    Siku chache baada ya Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kudai klabu tatu hazijamuunga mkono wakili wa kujitegemea, Dk Damas Ndumbaro aliyefungiwa kujihusisha na soka kwa miaka saba, klabu hizo zimeibuka na kusema haziungi mkono kukatwa makato yao ya udhamini. Kwa nyakati tofauti, viongozi wa Stand United, Coastal na Yanga wameeleza kutokubaliana na kukatwa asilimia tano ya mapato yao. Katibu Mkuu wa Coastal Union, Kassim El Siagi alisema Kamati isipotoshe, kwani wao hawakubaliani na kukatwa mapato yao hata asilimia moja, achilia mbali asilimia tano, na kwamba wapo pamoja na wenzao. Nye Katibu Mkuu wa Yanga, Benno Njovu alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema msimamo wao kuhusiana na hayo utatolewa baada ya viongozi wao kukutana hivi karibuni. Stand United kwa upande wao wapo kwenye mchakato wa kwenda kwa waziri wa michezo kushtaki kwamba hawakubaliani na makato hayo. Siku za karibuni kumeibuka mzozo baina ya Ndumbaro akiwa wakili wa klabu 12 za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya TFF. Mzozo huo ni baada ya TFF kuagiza kila klabu kukatwa asilimia tano za mapato yatokanayo na udhamini wa klabu hizo wanaoupata kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu ambao ni Vodacom na Azam Tv. Kamati ya Nidhamu ya TFF, chini ya makamu mwenyekiti wake, wakili Jerome Msemwa ilimfungia Ndumbaro kwa miaka saba kutojihusisha na masuala ya soka kwa madai ya kukiuka maadili ya kisheria kwa kushawishi, kupotosha, kutekeleza uamuzi wa TFF, kwa mujibu wa kanuni 41 (6).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako