• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serena Williams akosoa matamshi ya Shamil Tarpischev kumuita kaka

    (GMT+08:00) 2014-10-20 10:12:36

    Bingwa namba moja wa mchezo wa tenisi kwa upande wa akina dada duniani Serena Williams amekosoa matamshi ya rais wa shirikisho la Tenisi nchini Urusi Shamil Tarpischev, kwa kusema ni ya kibaguzi na kutojali ujinsia dhidi yake na dada yake Venus Williams. Katika mazungumzo yake Tarpischev aliwaita kina dada hao wawili kama ''kaka wawili''. Hata hivyo afisa huyo alipigwa faini ya pauni 15,500 na kupigwa marufuku ya mwaka moja kwa kutoa matamshi hayo aliyoyataja kama ya mzaha. Serena alisema matamshi hayo yalikuwa ni makali sana na wakati huohuo yamejaa ubaguzi. Matamshi ya Bwana Tarpischev pia yalilaaniwa na shirikisho la wanawake la mchezo wa Tenisi duniani WTA pamoja na shirikisho la mchezo huo nchini Marekani USTA. Katika taarifa yake Tarpischev ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Olimpiki ya kimataifa, amesema hakukusudia kumuudhi mwanariadha yeyote kwa maneno yake hayo, na kwamba anasikitika kwamba utani wake umesababisha kufuatiliwa sana na hafikirii tukio hilo linahitaji kuchukuliwa kama hivyo. Serena, 33, ameshinda mataji 18 ya Grand Slam, huku Venus mwenye miaka 34, akishinda 7.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako