• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wenger ajinasibu kuwa ubingwa ni wake safari hii

    (GMT+08:00) 2014-10-20 10:13:08

    Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema anatambua kikosi chake kimeachwa kwa pointi tisa na vinara Chelsea kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, lakini alisema hilo halimzuii kubeba ubingwa kwa msimu huu kwani nafasi ipo na ana kila sababu. Sare mbili za Leicester City, Everton na Tottenham zimeitibulia timu hiyo kwa msimu huu na sasa ipo kwenye nafasi ya nane baada ya kucheza mechi saba. Chelsea na Manchester City zipo kwenye nafasi za juu katika msimamo wa ligi hiyo, lakini Mfaransa huyo alisema anachokiona ni kwamba timu yake ina nafasi ya kubeba ubingwa wake wa kwanza baada ya kusubiri kwa miaka 11. Wenger anapiga hesabu ya kuipiku Chelsea kwenye usukani wa ligi hiyo lakini alipomenyana nao alikubali kichapo cha mabao 2-0 na hivyo kushindwa kupata ushindi kwa mara zote 12 alizokutana na Jose Mourinho kwenye maisha yake ya soka. Wakati huo huo, Wenger amefichua kwamba mwezi Januari lazima atafanya usajili mmoja mkubwa kukiboresha kikosi chake baada ya kushindwa kufanya hivyo kwenye dirisha la usajili lililopita. Wenger alifanya usajili wa nyota watano katika dirisha lililopita huku Alexis Sanchez akiwa staa wake mkubwa aliyemsajili kwa pesa nyingi akitokea Barcelona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako