• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Klabu ya Ugiriki yamkataza John Kamara kufanya mazoezi au kuchezea klabu yake kwa hofu ya Ebola

    (GMT+08:00) 2014-10-20 10:13:31

    Klabu ya Ugiriki PAS Lamia imemtaka mchezaji wa Sierra Leone John Kamara kutofanya mazoezi au kuchezea klabu yake kwa muda wa wiki tatu kutokana na hofu ya virusi vya Ebola. Kamara emerejea Ugiriki baada ya kuichezea timu yake ya taifa Leone Stars katika mechi ya kufuzu kucheza kombe la mataifa bingwa ya Afrika, mchezo ambao walitoka sare na Cameroon. Klabu hiyo imemwambia uamuzi huo unatokana na ushauri kutoka wizara ya afya ya Ugiriki. Uamuzi huo umetolewa na Lamar licha ya ukweli kwamba hakuna kesi za Ebola zilizoripotiwa nchini Cameroon na Kamara hakuwa nchini Sierra Leone kwa zaidi ya mwaka mmoja. Kamara amesema klabu yake imemwambia akae ndani asitoke nje au aende nchi za nje kutembelea familia yake lakini hatakiwi kwenda mazoezini. Hata hivyo klabu ilisisitiza uamuzi wake licha ya Kamara kuwaambia kuwa yuko tayari kuchukuliwa kipimo chochote wanachotaka. Kamara amesema inabidi afikirie hatma yake na klabu hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako