• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TFF na klabu za Tanzania kuomba muda zaidi kutafakari suala la makato

    (GMT+08:00) 2014-10-20 10:13:55

    Suala la makato ya asilimia tano kwa klabu za Ligi Kuu nchini Tanzania limechukua sura mpya baada ya kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na klabu kuomba muda zaidi kulitafakari. Kwenye mkutano ulifanyika juzi kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam pande zinazokinzana zimeafikiana kujadiliana zaidi zitakapokutana kwenye mkutano utakaofanyika baadaye ili kutoa uamuzi ya pamoja. Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi alisema klabu zimeonyesha kuridhishwa na wazo hilo, lakini zimeomba zipewe muda ili kujadiliana kwa kina. Kwa mtazamo wa wengine, suala hilo limetafsiriwa vibaya, kiasi cha kuchukua nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari, baada ya klabu kadhaa kati ya 14 zinazoshiriki Ligi Kuu kujitoa katika makubaliano ya awali huku Yanga ikikiri kutounga mkono au kupinga kukatwa kwa asilimia hiyo. Mbali na hilo, wakili wa kujitegemea ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya Ligi aliyekuwa akitetea klabu hizo kupinga kukatwa kwa asilimia hiyo, Dk Damas Ndumbaro amefungiwa miaka saba kujihusisha na masuala ya soka ndani ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako