• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • 22 wauwawa kwenye mlipuko Baghdad

    (GMT+08:00) 2014-10-20 10:15:16

    Watu 22 wameuwawa na wengine 25 wamejeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu la kujitoa mhanga uliolenga msikiti wa kishia mjini Baghdad Iraq.

    Wizara ya usalama wa ndani inasema huenda idadi ya vifo ikaongezeka kwani bado polisi wanaendela kuondoa majeruhi kwenye eneo hilo.

    Iraq imekuwa inashuhudia machafuko makubwa na Umoja wa mataifa unasema matukio ya ugaidi na mapigano vimesababisha zaidi ya watu 5, 500 kuuawa katika nusu ya kwanza ya mwaka huu.

    Hali ilianza kuwa mbaya zaidi mwezi juni yalipozuka mapigano kati ya maofisa wa usalama wa Iraq na kundi la ISIS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako