• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 4 wa Kamati kuu ya 18 ya chama cha kikomunisti cha China wafunguliwa leo

    (GMT+08:00) 2014-10-20 17:03:18

    Mkutano wa 4 wa Kamati kuu ya 18 ya chama cha kikomunisti cha China umefunguliwa leo hapa Beijing, kauli mbiu ya mkutano ni "utawala wa kisheria". Hii ni mara ya kwanza kwa mkutano huo kuweka mkazo katika utawala wa sheria tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango.

    Kwenye mahojiano ya mitaani, watu wa kawaida wameeleza kufuatilia mkutano huu wenye lengo la kuhakikisha utawala wa nchi unafuata sheria na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa usawa, furaha na heshima. Utawala wa kisheria kwa mara ya kwanza umekuwa ni ajenda kuu kwenye mkutano wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China.

    Mbali na kutafiti namna ya kusukuma mbele utawala wa kisheria na kuweka mpango wa kazi za uchumi katika nusu ya pili ya mwaka, jukumu lingine muhimu la mkutano huo ni kujadili ripoti ya kamati ya usimamizi wa nidhamu ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China na kufanya marekebisho ya uongozi. Wachambuzi wanaona kuwa mageuzi, utungaji sheria na mapambano dhidi ya ufisadi pia vitapewa kipaumbele kwenye mkutano huo.

    Katika mikutano 7 iliyopita ya kamati kuu ya chama tangu chama kianze kusimamia utekelezaji wa sera ya mageuzi na kufungua mlango, karibu yote ilitilia maanani ujenzi wa chama, pamoja na mageuzi ya makampuni ya kiserikali na masuala ya vijijini. Mkurugenzi wa idara ya utafiti wa historia ya chama katika chuo cha chama Bw. Xie Chuntao anaeleza ni kwa nini mkutano wa safari hii unazingatia utawala wa kisheria.

    "kwa sababu rais Xi Jinping amesisitiza kuwa mkutano si lengo kuu, lengo kuu ni kutatua masuala yaliyopo. China bado inakabiliwa na masuala mbalimbali katika utekelezaji wa sheria, kama vile baadhi ya idara za serikali zinatekeleza sheria ovyo au kwa uzembe, pia kuna masuala ambayo sheria hazijatekelezwa kwa usawa, na ufisadi katika utekelezaji wa sheria, wananchi hawawezi kuridhika kutokana na matatizo hayo. Naona kamati kuu ya chama imeweka ajenda kuu kwa kuzingatia hali hiyo."

    Tangu rais Xi Jinping aingie madarakani, mara nyingi amezungumzia masuala ya utawala wa kisheria. Kwenye mkutano wa kuadhimisha miaka 60 ya Bunge la umma la China, rais Xi alisisitiza tena umuhimu wa utawala wa kisheria kwa maisha ya wananchi na maendeleo ya nchi.

    "Tunapaswa kuimarisha kazi ya kutunga sheria zinazohusu sekta muhimu, kuhakikisha maendeleo ya nchi na mageuzi muhimu yote yanafuata sheria, na kuunganisha vizuri maamuzi yanayohusu maendeleo na mageuzi pamoja na maamuzi ya utungaji sheria, ili kukamilisha mfumo na utaratibu wa kutunga sheria, na kujitahidi kuhakikisha kila sheria inaendana na katiba ya nchi, inafuata nia ya wananchi na kuungwa mkono na wananchi. Tunapaswa kutekeleza kwa pande zote mikakati ya kuitawala nchi kwa mujibu wa sheria, kuhakikisha haki na usawa wa sheria, kuharakisha ujenzi wa nchi yenye utawala wa kisheria na kuhakikisha sheria zinatekelezwa kihalisi kwa haki na usawa na kuhakikisha kila raia anafuata sheria za nchi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako