• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia kuendeleza miradi 43 ya barabara kote nchini.

    (GMT+08:00) 2014-10-20 18:52:03

    Mamlaka ya ujenzi wa barabara nchini Ethiopia – ERA, imetangaza kuwa inatarajia kufanya miradi 43 ya barabara nchini humo, katika kipindi cha mwaka mmoja ujao wa kifedha.

    Miradi hiyo ya barabara kwa pamoja inatarajiwa kutumia Birr za Ethiopia bilioni 30.

    Kwa mujibu wa afisa mkuu wa uhusiano mwema katika mamlaka hiyo Samson Mondimu, ni kwamba asilimia 30 ya fedha hizo itagharamiwa na serikali ya nchi hiyo.

    Kati ya barabara hizo, barabara zinazotarajiwa kuundwa ni zile ambazo zinaunganisha majimbo muhimu humo nchini, pamoja na zile zinatumikia maeneo yaliyo na sekta muhimu za kiuchumi kama vile kilimo na utalii.

    Aidha barabara 31 kati ya 43 zitaundwa na makampuni ya humo nchini, na ni barabara 12 pekee ambazo zitaundwa na makampuni ya Kimataifa.

    Serikali inasema inatarajia kuendelea kuimarisha miundo mbinu humo nchini, hususan barabara katika harakati za kuchochea ukauji wa kiuchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako