• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Manchester United hali bado mbaya

    (GMT+08:00) 2014-10-21 11:18:40

    Baada ya mapumziko ya takribani wiki mbili, usiku wa jana jumatatu Manchester United wakasafiri kwenda kuumana na West Bromwich Albion katika mchezo wa raundi ya 8 wa Barclays Premier League. Mchezo uliopigwa katika dimba la Hawthorns umemalizika kwa klabu ya Manchester United kushindwa kupata matokeo chanya ugenini katika kipindi cha miezi zaidi ya 6, baada ya kutoka na sare ya 2-2. WBA ndio walianza kufunga katika dakika ya 8 kwa goli zuri la Sessegnon, goli hili likadumu mpaka mapumziko. Kipindi cha pili United walirudi kwa kasi na kufanikiwa kupata goli la kusawazisha kupitia Maroune Fellaini. Dakika kadhaa baadae Saido Beralinho akipafia WBA goli la pili, huku muda ukizidi kuyoyoma Daley Blind akaisawazishia Man United na kuipa sare ya 2-2. Wakati hayo yakijiri, meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesema lilikuwa ni jambo la kijinga kuwaambia watu kumweka kwenye mizani baada ya miezi mitatu tu tangu ajiunge na Manchester United kama kocha wa klabu hiyo. Tangu achukue usukani kama meneja wa Manchester United hapo Julai alipigiwa debe sana wengi wakisema kwamba mbinu zake zitaanza kuleta mafanikio baada ya miezi mitatu tu. Kufikia sasa miezi mitatu imeisha tangu ajiunge na Manchester United lakini timu hiyo bado inashikilia nambari ya sita katika orodha ya timu bora katika ligi ya kadanda ya Uingereza, huku ikiwa imeshindwa mechi mbili. Manchester United imeshinda mechi tatu zenye ushindani mkali tangu Van Gaal kujiunga na klabu hiyo msimu huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako