• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mchezaji wa soka nchini India afariki akisherehekea goli lake la ushindi

    (GMT+08:00) 2014-10-21 11:19:04

    Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao lake. Mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 23 na alijeruhi uti wake wa mgongo baada ya kupiga gema uwanjani akisherehekea bao lake la kusawazisha kwa timu yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari West FC. Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini baadaye alifariki. Mechi hiyo iliyomsababishia kupata jereha la mgongo, ilikuwa ni muhimu katika ligi ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako