Waziri wa michezo wa Afrika Kusini Fikile Mbalula amesema kama Morocco inajitoa nchi yake haitakuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwakani. Shirikisho la Soka Afrika CAF wiki iliyopita liliifuata Afrika Kusini, baada ya Morocco kuomba kutoandaa michezo hiyo kwa sababu za janga la Ebola. Amesisitiza kuwa huo ni uamuzi wa pamoja na kwa sasa bajeti ya Afrika Kusini hairuhusu kufanya hivyo. Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi saba zinazozingatiwa kuweza kuchukua nafasi ya Morocco kuandaa michuano hiyo iliyopangwa kufanyika kuanzia Januari 12 hadi Februari 6. Maofisa wa Morocco watakutana na Caf Novemba 3 kujadili suala hilo. Jibu lolote litakalopatikana, Afrika kusini tayari imeshaweka msimamo wake wazi. Afrika Kusini imeshakuwa mwenyeji mara mbili kwa dharura, ambapo ilichukua nafasi ya Kenya iliyokuwa na ukosefu wa pesa mwaka 1996 na Libya iliyokuwa ikisumbuliwa na vita mwaka uliopita, Ghana ni nchi nyingine inayotarajiwa kufuatwa na Caf, huku nchi nyingine tano zikiwa hazijawekwa wazi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |