Maprota wa ngumi nchini Kenya watalazimika kuweka pesa za zawadi za ushindi benki kupitia Shirikisho la ngumi za kulipwa la Kenya KPBC kabla ya kupewa leseni ya kuandaa pambano. Shirikisho hilo limesema limeanzisha sheria hiyo ili kuondoa mapromota wababaishaji, ambao badhi yao wamekuwa wakiwaibia mabondia kwa kukimbia na pesa zao. Akizungumza kwenye hafla ya kumtangaza mbunge wa kuteuliwa Johnson Sakaja, kama msimamizi wa KPBC ambaye anachukua nafasi ya Reuben Ndolo ambaye anagombea urais wa shirikisho la ndondi la Jumuiya ya Madola, mwenyekiti wa KPBC Hillary Alila, amesema shirikisho hilo linalenga kusaidia masuala ya mabondia kama njia moja wapo ya kufufua ndondi nchini humo. Sakaja amesema atashirikiana na kamati tendaji ya shirikisho hilo ili kuhakikisha yanakuwepo mapambano kila mwezi na kuvutia wadhamini mbalimbali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |