• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pistorius ahukumiwa miaka mitano jela

    (GMT+08:00) 2014-10-22 12:21:42

    Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp. Jaji aliyetoa hukumu hiyo, Thokozile Masipa alisema ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo. Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo apewe kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuua bila kukusudia. Pistorius alisema alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumbani kwake. Upande wa mashitaka ulisisitiza Pistorius afungwe jela wakati mawakili wa Pistorius wakimtaka jaji ampe kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake. Jaji alisema Pistorius asingepewa adhabu ya kifungo cha nyumbani kwani hukumu kama hiyo ingekuwa hatua mbaya na mfano mbaya kwa wahalifu. Wazazi wa Reeva Steenkamp kwa upande wao walifurahia hukumu ya jaji na pia kuridhika kwamba kesi hiyo imekamilika. Mwanariadha huyo wa kimataifa hataruhusiwa kukushiriki mashindano yoyote ya riadha kwa miaka mitano atakayokuwa jela hata ikiwa ataachiliwa kabla ya miaka hiyo kukamilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako