• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiplagat asema wanariadha wa Kenya wanalengwa kwa njia zisizo za haki

    (GMT+08:00) 2014-10-22 12:22:50

    Mwenyekiti wa wanariadha wa Kenya Isaiah Kiplagat amesema mchezo wa riadha unalengwa kwa njia zisizo za haki na wao ndio wanaoathirika kupata mafanikio kimataifa katika mbio ndefu na fupi. Hata hivyo Kiplagat ambaye alikuwa akiongea huko Eldorent, hakukanusha kuhusu wasiwasi ulioibuliwa na shirika la kuzuia dawa za kuongeza nguvu WADA, na ripoti za waandishi wa habari ambazo zinathibitisha kuenea kwa dawa hizo. Kenya itatuma timu ya wataalamu wa kupambana na dawa za kuongeza nguvu kwenye shirika la kupambana na dawa za kuongeza nguvu la Afrika, huko Cape Town baadaye wiki hii, kuhudhuria mkutano wa nchi tatu pamoja na mashirika ya kupambana na dawa za kuongeza nguvu ya Norway na China utakaojadili namna ya kutokomeza dawa hizo. Hata hivyo kukataa kwake Kiplagat na wanariadha wote wa Kenya kufanyiwa mahojiano na kamati iliyoteuliwa na wizara ya michezo inayoangalia sakata la dawa za kuongeza nguvu, kumezua hisia tofauti juu ya wanachokificha wanamichezo hao. Tangu hapo WADA imewasimamisha zaidi ya wanariadha 30 wa Kenya kwa kukamatwa na dawa hizo tangu mwaka 2005.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako