Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya Uefa Michael Platini, ametaka kuombwa radhi baada ya Shirikisho la Soka la Afrika kumkosoa kwa maoni yake juu ya kupanga michuano ya kombe la mataifa ya Afrika. Caf imemshutumu Platini kwa kitendo chake cha kuingilia kati baada ya kujadili athari ya ugonjwa wa Ebola katika michuano hiyo kupitia televisheni. Hata hivyo rais huyo wa Uefa anasisitiza kuwa maoni yake yametafsiriwa vibaya huku Caf ikisema Platini asitegemee kabisa kama ataombwa msamaha. Caf ilitowa taarifa kali siku ya Jumanne ikimkosoa Platini, ambaye wanadai alipendekeza kwenye mahojiano hayo, kuwa michuano hiyo iahirishwe, madai ambayo Platini ameyakanusha. Caf imesisitiza kuwa haitamruhusu mtu yoyote kuingilia usimamizi wa mambo yake.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |