Mwamuzi wa mchezo wa masumbwi Mageja Dziurgota amepelekwa hospitalini huko Croatia kupata matibabu baada ya kujikuta akishushiwa makonde ya kutosha na bondia Vido Loncar mwenye miaka 18, aliyekuwa akipambana na bondia kutoka Lithuania, Algirdas Baniulis. kizaazaa hicho cha mwaka kimemkuta mwamuzi huyo mara baada ya kumtangaza Baniulis kuwa mshindi katika pambano hilo. Shirikisho la mchezo wa masumbwi limemfungia bondia huyo kucheza pambano lolote, japo wanaamini kuwa bondia huyo si 'mnyama' kama anavyodhaniwa na watu baada ya kumtwanga makonde mwamuzi huyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |