• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vurugu na ghasia zaguigubika Ligi ya Kenya

    (GMT+08:00) 2014-10-23 12:27:53

    Msimu wa ligi kuu ya soka nchini Kenya ukiwa unaelekea ukingoni, ushindani mkali uliopelekea vurugu umesababisha mechi mbili kuvunjwa wiki iliyopita mjini Nairobi. Shirikisho la soka la Kenya FKF limesema litatoa adhabu kali dhidi ya pande husika zilizosababisha vurugu za kuwania taji la ligi kuu ya Kenya kati ya Tusker FC na Muhoroni Youth siku ya Jumamosi usiku pamoja na vurugu zilizotokea chini ya saa 24 kwenye nusu fainali kati ya AFC Leopard na Sofapaka. Mabingwa wa ligi hiyo wataiwakilisha Kenya katika msimu mpya wa ligi ya mabingwa ya Caf huku washindi wakiendelea mbele katika mashindano mengine ya bara na kombe la shirikisho la CAF. Siku ya jumapili, uwanja wa Nairobi uligubikwa na vurugu ambazo zimewafanya polisi kutuliza vurugu zilizofanywa na mashabiki wa AFC walikuwa na hasira kali baada ya kufungwa na Sofapaka kwa mabao 2-0.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako