• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sir Alex Ferguson amkana kabisa David Moyes

    (GMT+08:00) 2014-10-24 10:04:51

    Aliyekuwa kocha Manchester United Sir Alex Ferguson amemkana kabisa kocha aliyerithi kiti chake, David Moyes, ambaye aliishia kuondolewa klabuni hapo kwa aibu kubwa. Kwanza kabisa, Ferguson amedai kuwa hakuhusika peke yake katika mchakato wa kumchagua Moyes kuwa kocha wa timu hiyo, lakini hapo hapo akadai kwamba kocha huyo hakujua ukubwa wa Manchester United. Ferguson ameandika maelezo mapya katika kitabu cha maisha yake na kuna matukio yaliyotokea siku za karibuni ambayo ameyaingiza katika kitabu hicho likiwamo suala la kustaafu kwake na ujio wa Moyes. Ferguson mzaliwa wa Scotland mwenye umri wa miaka 72, pia amehoji maamuzi ya Moyes kufukuza watu wake wote aliowaacha Old Trafford pamoja na msaidizi wake wa muda mrefu, Mike Phelan, na kukumbusha kuwa presha ambayo Moyes aliipata kwa vichapo mbalimbali ilikuwa sawa na ile ambayo yeye mwenyewe aliipata mwaka 1989 wakati timu hiyo ilipokaribia kushuka daraja kabla hajaibuka kupata mafanikio.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako