Mkufunzi wa Liverpool Brendan Rogers amemkumbusha mshambuliaji wa timu hiyo Mario Baloteli kuhusu utamaduni wa soka ya Uingereza na hususan ule ya Liverpool. Baada ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza cha mechi kati ya Real Madrid na Liverpool, mchezaji huyo raia wa kitaliano alibadilishana jezi yake na mchezaji wa Liverpool Pepe Reina. kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Adam Lallana katika mechi ya UEFA. Wakati huo tayari Liverpool ilikuwa imefungwa mabao matatu kwa bila. Rogers alisema alijadiliana na Baloteli kuhusu utamaduni wa ligi ya Uingereza na Liverpool na kumuomba ajitahidi kufanya mambo mazuri. Baloteli anafanya juhudi za kuimarisha ushambuliaji wake ambapo amefunga bao moja pekee katika mechi kumi. Hata hivyo mchambuzi wa soka wa BBC anaamini kuwa Rodgers anapaswa kumpiga faini mchezaji huyo na kumtema kwenye timu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |