• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vituko: Messi agoma kubadilishwa kiwanjani walipocheza na Liverpool

    (GMT+08:00) 2014-10-24 10:05:41

    Nyota wa soka, Lionel Messi, ameripotiwa kumgomea kocha wake Luis Enrique wakati alipotaka kumtoa kwenye mechi kati ya Barcelona na Eibar. Gazeti la AS limeripoti kwamba wakati kikosi chake kikiwa mbele kwa mabao 3-0, kocha huyo wa Barca alipanga kumtoa Messi ili amwingize Munir El Haddadi kwenye dakika ya 76. Luis Enrique alisimama nje ya mstari na kuonyesha ishara kwamba Muargentina huyo anapaswa kutoka, lakini Messi aligomea amri ya kocha wake na kuendelea kubaki uwanjani. Baada ya kuona mpango huo umekwama, Enrique aliamua kumtoa Neymar na kumwingiza Munir. Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Enrique alisema ni lazima aweke sawa kila kitu, lakini anaamini katika hisia zake kuwa kwa sasa kitu muhimu ni timu na pia Messi mwenyewe. Kocha huyo amekiri kuwa wana bahati kwa kuwa na Messi kwenye timu yao. Juzi Jumanne kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, Barcelona iliichapa Ajax mabao 3-1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako