• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha wa timu ya Rugby ya Kenya akosoa ripoti inayomhusisha na dawa za kuongeza nguvu

    (GMT+08:00) 2014-10-24 10:06:49

    Kocha mkuu wa timu ya Rugby nchini Kenya Treu amesema ripoti iliyotolewa na shirika linalodhaminiwa na serikali linalopambana na dawa za kuongeza nguvu ambayo inamtuhumu yeye na benchi lake la ufundi kwa kuanzisha kuanzisha vyakula vilivyogundulika kuwa na steroid baada ya kujaribiwa. Kwenye taarifa iliyotumwa na Glenda Neville kutoka Afrika Kusini kwa niaba yake, Treu amekanusha kuanzisha vyakula hivyo, akidai kuwa yeye ndiye anayehusika na kuanzisha sera ya vyakula visivyo na chembe za dawa wakati alipowasili nchini Kenya mwezi Novemba mwaka jana kuifundisha timu hiyo. Kikosi kinachoongozwa na profesa Moni Wekesa, kimekamilisha ripotiu yake ya awali mwezi Aprili, lakini ilitolewa rasmi na mawaziri wa michezo, sanaa na utamaduni wa Kenya Dkt Hassan Wasio ijumaa iliyopita. Treu amehoji sifa ya wachunguzi ambao hawatambuliwi na Bodi ya kimataifa ya Rugby kama shirika la kupambana na dawa za kuongeza nguvu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako