China imerusha chombo kisichobeba mtu kwenye anga ya juu leo alfajiri kwa ajili ya kuifanyia majaribio teknolojia itakayotumiwa kwenye chombo cha Chang'e-5, kinachotarajiwa kurushwa na China kwenye sayari ya mwezi na kurudishwa duniani.
Mwezi Desemba mwaka jana, China ilifanikiwa kurusha chombo cha Chang'e-3. Chombo hicho kilichobeba chombo cha kufanya utafiti kinachojulikana kama Yutu kilitua salama kwenye mwezi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |