• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yarusha chombo cha majaribio cha kuchunguza mwezini

    (GMT+08:00) 2014-10-24 17:54:09

    China imerusha chombo cha majaribio cha kuchunguza mwezini ambacho kinatarajiwa kurejea ardhini kwa kutumia roketi ya Changzheng No. 3E kutoka kituo cha kurushia saitelaiti cha Xichang. Jukumu la chombo hicho ni kufanya majaribio ya teknolojia na kukirejesha ardhini, pia kusaidia chombo cha kuchunguza mwezini Chang'e No.5.

    Saa nane kamili leo alafajiri, roketi ya Changzheng No. 3E iliyobeba chombo cha majaribio cha kuchunguza mwezini imerushwa, baada ya sekunde kadhaa, chombo hicho kikaachana na roketi na kuingia kwenye njia yake yenye umbali wa kilomita 209 kutoka duniani.

    Jaribio hilo ni la mara ya kwanza kwa China kurusha chombo cha anga ya juu kinachotarajiwa kurejea ardhini. Naibu mkurugenzi wa Idara kuu ya safari ya anga ya juu ya China Wu Yanhua amesema, baada ya kurushwa kwa chombo hicho, kitaruka kwa vipindi vitano katika siku 8 zijazo.

    "urushaji wa mafanikio ni hatua moja muhimu katika majaribio hayo, kwa mujibu wa mpango, chombo hicho kitaruka kuelekea mwezini, kuzunguka mwezi, kuondoka mwezi na hatimaye kurejea ardhini."

    Chombo hicho cha majaribio kinaundwa kwa sehemu mbili, sehemu ya kurejea ardhini na sehemu ya huduma. Sehemu yake ya huduma inatumia teknolojia ya Chombo cha Chang'e No.2 na hata umbo lake linafanana na Chang'E No.2. Sehemu ya kurejea ardhini inafanana na chombo cha Shenzhou, lakini ni ndogo zaidi, ukubwa wake ni 1/8 ya chombo cha Shenzhou.

    Baada ya siku nane, sehemu ya kurejea ardhini tu ya chombo hicho ndio itakayorudi, bila sehemu ya huduma. Akifafanua safari ya chombo hicho kwenda na kurudi kutoka mwezini, Naibu msanifu mkuu wa mfumo wa chombo hicho Bw. Zhang Wu, anasema

    "Sehemu ya kurejea na sehemu ya huduma zote zitarushwa kwa pamoja kuelekea mwezini, zitazunguka mwezi halafu kurudi ardhini. Baada ya kufika mahali pa kuingilia kwenye njia ya kurejea ardhini, sehemu hizo mbili zitatengana, sehemu ya huduma haitarudi ardhini, na sehemu ya kurejea itafuata njia ya kuelekea ardhini. Katika mchakato huo, sehemu ya huduma inatoa umeme kwa ajili ya sehemu ya kurejea, na pia inasimamia na kudhibiti sehemu ya kurejea ardhini."

    Akifafanua lengo la majaribio hayo, Naibu mkurugenzi wa Idara kuu ya safari za anga ya juu ya China Wu Yanhua, amesema:

    "Tunataka kupata data kamili za majaribio, ili kutoa uungaji mkono muhimu kwa mradi wa Chang'E No.5, kuthibitisha teknolojia mpya, usanifu mpya na mpango mpya utakaotumika katika Chang'E No.5, kuhakikisha mafanikio ya chombo cha Chang'E No. 5 kinachotarajiwa kurushwa mwaka 2017, na kuweka msingi wa kiteknolojia na kukusanya uzoefu wa miradi kwa ajili ya kazi za uchunguzi wa anga ya juu katika siku zijazo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako