• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kigali Rwanda:EAC yashauriwa kuwekeza katika elimu

    (GMT+08:00) 2014-10-24 19:55:16

    Wataalamu waliohudhuria kongamano la sekta za umma na zile za kibinafsi Kigali Rwanda wametoa mwito kwa wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki kuwekeza katika masomo ili kuboresha fursa za ajira.

    Sekta za kibinafsi zimetakiwa kushirikiana zaidi na vyuo vikuu kufanya utafiti wa ubunifu wa ajira kwa lengo la kukuza vipaji kutoka kwa wanafunzi.

    Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Richard Sezibera amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kutafuta ujuzi wa teknolojia ya kisasa miongoni mwa wanachama wa EAC.

    Sezibera amesema EAC haitaweza kufikia malengo yake kama kutakosekana ujuzi wa kutosha katika sekta za elimu na biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako