• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mambo yazidi kuwa mabaya kwa Mario Balotelli dhidi ya Liverpool

    (GMT+08:00) 2014-10-27 11:35:19

    Hali imezidi kuwa mbaya kwa nyota mtukutu wa Liverpool, Mario Balotelli, baada ya taarifa za ndani ya klabu yake kusema kuwa mchezaji huyo atawekwa sokoni Januari. Imeelezwa kwamba viongozi wa klabu hiyo hawatajali hasara ya kumnasa mchezaji huyo kwa Pauni milioni 16 katika dirisha la usajili lililopita. Balotelli ambaye alihamia Liverpool akitokea AC Milan alishindwa kutamba kwenye timu yake ya awali, lakini kocha Brendan Rodgers alitegemea nyota huyo angebadilika. Hata hivyo sikio la kufa halisikii dawa, ubovu wa Balotelli umejionyesha wazi. Tangu msimu huu ulipoanza, nyota huyo amefunga bao moja tu jambo ambalo si sahihi kwa mshambuliaji wa kati. Katika kupigilia msumari wa moto, nyota wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher, amesema haoni sababu yoyote ya kuendelea kumfuga mchezaji huyo ambaye haonyeshi ushindani. Carragher alisema kuwa anatarajia kuona klabu hiyo ikimtimua Balotelli kabla ya kuanza msimu ujao. Carragher ambaye hakufurahishwa na kasi ndogo ya nyota huyo kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid Jumatano wiki iliyopita ambapo Liverpool ilichapwa mabao 3-0, alisema Mario hawezi kubadilika, yeye ni mtukutu, labda alivumiliwa alipokuwa Machester City kwa sababu alikuwa akifunga mabao. Katika hatua nyingine, kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, amesema hakuna sababu ya kumtupia lawama Balotelli kwa kuwa si yeye peke yake aliyecheza vibaya. Alisema wachezaji kadhaa wa Liverpool walicheza chini ya kiwango.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako