• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mark Kiptoo ang'ara kwenye mbio za Frankfurt

    (GMT+08:00) 2014-10-27 11:36:09

    Mwanariadha wa Kenya Mark Kiptoo ameimarisha ushindi wake katika mashindano ya mbio za Frankfurt mwaka huu baada ya kuibuka mshindi. Kiptoo mbaye alimaliza katika nafasi ya pili mwaka uliopita aliwaongoza wanariadha wengine wa Kenya kushinda nafasi tatu bora katika mbio za wanaume. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 38 ambaye alishinda medali ya shaba katika mbio za mita 5000 katika mashindano ya Jumuiya ya Madola, alimaliza mbio hizo akitumiua muda wa saa 2, dakika 6 na sekunde 49, katika mbio za kusisimua ambazo ziliamuliwa ikiwa imesalia kilomita moja. Mike Kigen alimaliza katika nafasi ya pili kwa saa 2 dakika 6 na sekunde 59 naye Gilbert Yegon akawa wa tatu kwa kutumia saa 2 dakika 7 na sekunde 8 baada ya bingwa mtetezi pia kutoka Kenya kupoteza uongozi na kundi la kwanza katika kituo cha kilomita 30.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako