• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Moyes karibu kung'ong'ona nofu kwenye timu ya Inter Milan

    (GMT+08:00) 2014-10-28 12:29:25

    Kocha David Moyes, amewekwa kwenye mikakati ya kuinoa Inter Milan baada ya klabu hiyo ya Italia kufikiria kuachana na Walter Mazzarri. Kwa sasa Inter Milan inavutavuta tu muda na kocha Mazzarri na kwamba inaweza kumtupia virago vyake muda wowote kutokana na timu hiyo kufanya vibaya kwenye Ligi Kuu Italia 'Serie A'. Moyes, aliyewahi kuzinoa Manchester United na Everton, anapewa nafasi kubwa ya kumrithi Mazzarri ambaye yupo kwenye kitimoto na timu yake ambayo juzi Jumapili ilicheza dhidi ya Cesena. Licha ya Moyes kudai kwamba itambidi afikirie sana kufundisha timu ya nje ya England, lakini ofa ya kufanya kazi Inter Milan inaweza kumvutia na akachukua kibarua hicho. Rais wa zamani wa Inter, Massimo Moratti, alijiuzulu cheo hicho Ijumaa iliyopita akiweka hadharani wasiwasi wake juu ya uwezo wa kocha Mazzarri jambo ambalo linatoa nafasi kubwa kwa Moyes kupewa ajira mpya. Mmiliki mpya wa klabu hiyo, Erick Thohir, ndiye anayeendelea kumvumilia kocha huyo wa zamani wa Napoli.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako