• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kilimo cha chai chawaongezea kipato wakulima wa kijiji cha Tianba mkoani Guizhou

    (GMT+08:00) 2014-10-29 09:29:13

    Katika kijiji cha Tianba mjini Zunyi mkoani Guizhou, China, Chen Qibo, mkulima anayejishughulisha na kilimo cha chai kwa zaidi ya miaka 30 alimwambia mwandishi wetu wa habari kwamba, katika miaka ya 80 karne iliyopita, mimea haikustawi katika kijiji chake, lakini sasa kilimo cha chai kimewaletea wakulima wa huko mapato mengi.

    Kijiji cha Tianba kiko umbali wa kilomita moja hivi kutoka usawa wa bahari. Asilimia 85 ya ardhi inafunikwa na misitu. Kijiji hiki kina mashamba ya chai zaidi ya hekta 1,300. Karibu kila familia ya wakulima ina shamba la chai. Ukisimama katika mlima Xianren kijijini humo, utaona mashamba ya chai na nyumba za wakulima zimetapakaa misituni, na wakulima wengi wanapalilia mashamba yao.

    Bw. Chen anasema, wakulima wanapalilia kwa mikono badala ya kutumia dawa za kemikali, pia wanaua wadudu kwa kutumia karatasi za kunatanata, hivyo chai zinazozalishwa huko hazina uchafuzi.

    Habari zinasema, chai zinazozalishwa kijijini Tianba zimefikia vigezo zaidi ya 400 vya usalama wa chakula vya Umoja wa Ulaya, na zinauzwa katika nchi mbalimbali ikiwemo Ujerumani.

    Katika miaka ya hivi karibuni, wateja wanatilia mkazo zaidi usalama wa chakula, chai zisizo na uchafuzi zinafurahiwa zaidi sokoni, na zimewaongezea wakulima kipato zaidi. Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, mauzo ya rejareja ya chai ya kijijini humo yalikuwa karibu yuan milioni 30, na wastani wa kipato kwa kila familia ni zaidi ya yuan elfu 10.

    Lakini katika miaka 10 iliyopita, hali ya kijiji hiki ilikuwa tofauti kabisa. Bw. Chen anasema ilikuwa ni vigumu kweli kwa kijiji chake kupata mafanikio makubwa kutokana na kilimo cha chai. Familia yake ni ya kwanza kujishughulisha na kilimo cha chai kijijini hapo, lakini wakulima wengi hawakutaka kufanya shughuli hiyo kwa sababu hawakuwa na uhakika kama kilimo cha chai kitawapatia kipato au la.

    Mwaka 2001, Bw. Chen aliwapatia wanakijiji wengine mimea ya chai, na waliilipia baada ya kuuza chai. Idara husika za serikali za ngazi mbalimbali pia zimetangaza kuunga mkono kilimo cha chai, na mashamba ya chai yameongezeka siku hadi siku.

    Mkurungezi wa kituo cha huduma za usimamizi wa utalii cha kaunti ya Fenggang Bw. Chen Yunlong amefahamisha kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, kaunti hiyo imefanya majaribio ya kusukuma mbele kilimo cha chai na utalii kwa pamoja.

    Chen Qibo ana matarajio makubwa kuhusu maendeleo ya utalii katika kijiji chake. Ametangulia tena kufanya kazi hii kwa kuanzisha duka la chai na hoteli. Anasema watalaiii si kama tu wanaweza kuonja chai na kupumzika, bali pia wanaweza kula vyakula vilivyopikwa kwa chai na kushiriki wenyewe kwenye uzalishaji wa chai.

    Hivi sasa hatua za kushirikisha kilimo cha chai na utalii zimepata mafanikio, na mapato ya wakulima yanaendelea kuongezeka. Habari zinasema eneo la kitalii limewaajiri zaidi ya watu 500, bei ya chai imeongezeka na kufikia zaidi ya yuan 200 kwa kilo kutoka zaidi ya yuan 20 zamani, na wastani wa kipato kwa kila mkulima imefikia yuan elfu 10 sasa kutoka yuan 2000 mwaka 2000.

    Bw. Chen Yunlong anasema, si kama tu kilimo cha chai kimeboresha mazingira ya kiasili, bali pia kimeongeza kipato cha wakulima, utalii umeboresha muundo wa shughuli za kilimo, na kutoa mchango katika utoaji wa nafasi za ajira. Chen Qibo anatarajia kwamba, idara husika za serikali zitaongeza nguvu katika kuboresha mazingira ya huko na kuyahifadhi mashamba ya chai, ili yawapatie wakulima wa huko faida kubwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako