• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FIFA: Mashindano ya kombe la dunia ngazi ya vilabu kuendelea

    (GMT+08:00) 2014-10-29 10:28:49

    Shirikisho la soka Duniani FIFA limesema mashindano ya kombe la dunia la FIFA kwa ngazi ya vilabu yanayotarajiwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu yataendelea kama ilivyopanga, huku likivisisitiza vilabu vyote kuchukua tahadhari juu ya virusi vya Ebola pindi inapofanyika michuano hiyo ya kimataifa. Kitendo cha baadhi ya nchi kukumbwa na janga la Ebola kiliibua maswali namna ambavyo michuano hiyo itawezekana kufanyika na pia juu ya usalama wa wachezaji hasa pale ambapo watalazimika kwenda kucheza mechi katika moja ya nchi ambayo iko kwenye ukanda ulioathirika na ugonjwa huo. FIFA imewatoa wasi wasi kwa kutoa ushauri namna ambavyo itasaidia kupunguza hatari ya kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa huo. Mbali ya mapendekezo yaliyotolewa na FIFA ya kufanya vipimo vya afya za wachezaji wa vilabu husika baada ya kurejea kutoka moja ya nchi ambayo iko katika ukanda ulioathiriwa na Ebola, pia imeshauri baadhi ya mechi ambazo zilipangwa kufanyika Guinea, Sierra Leone na Liberia kuhamishiwa katika viwanja vya nchi nyingine. Mbali na FIFA kusisitiza kuwaweka haraka kwenye karantini wachezaji watakaoonesha dalili za Ebola wakati ikifanyika michuano ya kimataifa, vile vile imewataka wachezaji kutoka nchi zilizoathirika kuwa na tahadhari kubwa ya kupima afya zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako