• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afisa wa shirikisho la soka la Northumberland, Uingereza aadhibiwa kwa kumkebehi refa mwanamke

    (GMT+08:00) 2014-10-30 11:14:15

    Makamu wa Rais wa shirikisho la soka katika kiunga cha Northumberland, Uingereza John Cummings amesimamishwa kwa kipindi cha miezi 4 kwa kosa la kumwambia mwamuzi wa kike kuwa sehemu anayopaswa kuwapo mwanamke ni jikoni na sio katika uwanja wa soka. Cummings amemtolea kauli hiyo mwamuzi Lucy May, kwamba hawezi kuhimili kazi ya kuwa mwamuzi, na kuongeza kuwa katika maisha yake yote hakuwahi kuona mwanamke akichezesha soka. Tume huru ya uratibu wa shirikisho la soka imesema kuwa Cumming amekiuka kanuni za soka za shirikisho hilo kwa kutumia lugha ya kukashifu na ubaguzi wa kijinsia. Makamu huyo wa rais amekiri kuwa hakuwa anamaanisha kile alichokizungumza bali ilikuwa ni utani ambao huenda May hajauchukulia hivyo, japo chama hicho kimesema nafasi ipo wazi kwa refarii huyo kukata rufaa juu ya hukumu hiyo. Hukumu aliyopewa refa huyo inaambatana na adhabu ya faini ya paundi 250 na pia adhabu ya kuhudhuria mafunzo. Mkurugenzi wa chama cha soka Northumberland, Clive Oliver amekemea kitendo hicho na kusema soka unajumuisha watu wote na hakuna ubaguzi wowote unaopaswa kuvumiliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako