• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Klabu kubwa za Ulaya zataka michuano ya Qatar kufamyika kuanzia Aprili hadi Mei

    (GMT+08:00) 2014-10-31 11:05:33

    Klabu kubwa barani Ulaya zitakutana wiki ijayo kwa lengo la kuliomba Shirikisho la Soka duniani FIFA kuandaa michuano ya kombe la dunia nchini Qatar kati ya tarehe 28 mwezi Aprili na 29 mwezi Mei mwaka 2022. Qatar imekabidhiwa kuandaa michuano hiyo mwaka 2010 lakini hoja za kubadilisha michezo hiyo katika miezi ya joto kali, zimekuwa zikitolewa. Muungano wa vilabu vya Ulaya, zikiwemo Manchester, Liverpool, Barcelona na Bayern Munich unataka kuwasilisha ombi hilo ikiwemo kuanza mechi za ligi ya msimu wa mwaka 2021 na 2022 wiki mbili kabla na kucheza mechi za mwisho za kombe la FA baada ya fainali za kombe hilo. Kwa kuwa kombe la dunia limepangwa kufanyika Mei 29, hii itasababisha kombe la FA nchini Uingereza kukamilika mwezi Juni. Muungano huo unaowakilisha timu kubwa 214 za bara Ulaya, unaamini kuwa michuano hiyo ambayo inaweza pia ikaathiri mashindano ya mataji ya nyumbani nchini Ufaransa na Hispania, itabadilishwa tarehe. Hata hivyo Uefa inapendelea zaidi michuano ya Qatra kuchezwa Januari na Februari 2023.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako