• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mastaa wa soka wa Hispania kwenda tena Tanzania

    (GMT+08:00) 2014-10-31 11:05:57

    Nyota wa zamani wa Barcelona, Patrick Kluivert, Rivaldo na Deco wanatarajiwa kukiongoza kikosi cha wachezaji wa zamani wa Barcelona kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya kikosi cha wakongwe wa soka nchini Tanzania mwezi Desemba. Ziara hiyo ya nyota wa klabu maarufu za Hispania itakuwa ya pili kufanyika nchini humo baada ya wale wa Real Madrid kuzuru vivutio vya utalii hivi karibuni na kuwachapa wakongwe wa Tanzania mabao 3-1 mbele ya Rais Jakaya Kikwete. Akithibitisha ujio wa wachezaji hao akiwa nchini Hispania, Mkurugenzi Mkuu wa TSN Group, Farough Baghozah alisema kampuni yake ipo katika hatua za mwisho kuwapeleka wakongwe hao. Naye Kluivert ametoa wasiwasi watu kwa kusema atafuatana na kikosi cha wakongwe wenzake wa Barcelona katikati ya Desemba kwa ajili ya pambano hilo. Agosti 24, TSN ilifanikiwa kuwapeleka wakongwe wa Real Madrid wakiongozwa na Louis Figo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako