• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nigeria yatengua hukumu yake kuepuka kufungiwa na Fifa

    (GMT+08:00) 2014-10-31 11:06:22

    Nigeria inatumai kuwa itapeuka marufuku kutoka kwa Shirikisho la Soka Duniani Fifa baada ya mahakama kutengua uamuzi wake wa hivi karibuni wa kubatilisha uchaguzi wa shirikisho la soka la Nigeria uliofanyika mwezi uliopita. Nigeria ilipewa hadi leo ijumaa kutengua hukumu yake iliyotolewa na mahakama kuu ya Jos ambayo ilibatilisha uchaguzi huo uliofanyika septemba 30 na kumshuhudia Amaju Pinnick akiwa rais wa shirikisho hilo. Rais Goodluck Jonathan juzi aliingilia kati ili kumaliza mgogoro huo. Fifa bado haijathibitisha kama Nigeria itaepukana na marufuku hiyo ambayo kama watapewa itamalizika mwezi Mei mwakani. FIFA iliionya nchi hiyo juzi jumanne kwamba vitendo kama hivyo haviruhusiwi kwenye sheria zake na kinahatarisha nchi kupigwa marufuku kushiriki soka ya kimataifa kwa muda mrefu. Juzi jumatano rais Jonathan alikuwa na mazungumzo na wahusika wakuu wawili katika mzozo huo wa NFF, rais anayetambuliwa na Fifa na Amaju Pinnick na mtu anayesema anapaswa kuwa rais wa shirikisho hilo Chris Giwa. Baadaye rais alimuamuru Gira na washirika wake waliopelekea kumpindua Pinnick kujitoa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako