• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya bidhaa ya Afrika Kusini ya mwaka 2014 yafunguliwa Beijing

    (GMT+08:00) 2014-10-31 11:19:14

    Maonesho ya bidhaa ya Afrika Kusini ya mwaka 2014 yamefunguliwa hapa Beijing. Maonesho hayo yameonesha mazingira na sera ya uwekezaji ya Afrika Kusini, na miradi ya kuvutia wafanyabiashara. makampuni yanayoshiriki kwenye maonesho hayo yanajihusisha na sekta za uzalishaji wa kilimo, viwanda vya kemikali, magari, nishati na nishati endelevu, mawasiliano ya habari.

    Waziri wa biashara na viwanda wa Afrika Kusini Bw. Rob Davies ameeleza matumaini kuwa Afrika Kusini na China zitashirikiana kwa karibu katika sekta za teknolojia ya kilimo, ubunifu wa bidhaa za viwanda na sayansi na teknolojia ya juu. Amesema Afrika Kusini itaboresha na kukamilisha zaidi mazingira ya uwekezaji kwa wafanyabiashara wa nchi za nje, na kutoa sera nafuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako