• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya waondoa vikwazo vya kiuchumi vya miaka 12 dhidi ya Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2014-10-31 11:20:05

    Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Zimbabwe Philipe Van Damme ametangaza kuwa Umoja wa Ulaya umeamua kuondoa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Zimbabwe, hivyo Zimbabwe itapata tena msaada wa kiuchumi kutoka umoja huo kuanzia mwaka kesho.

    Bw. Van Damme amesema vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Zimbabwe vitaondolewa rasmi tarehe 1 Novemba, na umoja huo unapanga kutoa msaada wenye dola za kimarekani milioni 234 kwa Zimbabwe kati ya mwaka 2015 na 2020 kwa ajili ya kuisaidia serikali ya Zimbabwe kuboresha mazingira ya matibabu na kuwekeza katika sekta ya kilimo, kuimarisha ujenzi wa idara na uwezo wa usimamizi, na kuendeleza mashirika yasiyo ya kiserikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako