• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Manchester United yarambwa 1-0 na mahasimu wao Manchester City

    (GMT+08:00) 2014-11-03 10:18:47

    Ligi kuu ya soka England imeendelea kwa michezo miwili iliyopigwa kwenye jiji la Manchester na jijini Birmingham ambapo kwenye mchezo wa kwanza Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Manchester City waliwafunga mahasimu wao wa jadi Manchester United moja kwa bila kwenye uwanja wa Etihad. Bao pekee lililoamua mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji raia wa Argentina Sergio Kun Aguerro ambaye alimalizia pasi ya Gael Clichy. United katika mchezo huo ilimaliza ikiwa pungufu baada ya mlinzi Chris Smalling kuonyeshwa kadi nyekundu mapema kwenye kipindi cha kwanza ambapo hata hivyo matatizo ya United hayakuishia hapo kwani baadaye mlinzi wa kimataifa wa Argentina Marco Rojo alilazimika kutolewa nje baada ya kuumia bega. Huu ni ushindi wa nne mfululizo ambao City inaupata mbele ya United huku Sergio Aguerro akiendelea kuwaumiza mashetani wekundu akiwa tayari amefunga magoli matano kwenye michezo sita dhidi ya United. Naye kocha wa Man United Louis van Gaal amekasirishwa kwa kitendo cha kutolewa Smalling akisema ni kitendo cha kipumbavu. Smalling alitolewa kabla ya mapumziko kwa madhambi mawili ikiwemo kumgonga mlinda mlando wa City na pili kutafuta ugomvi dhidi ya James Miller.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako