• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachezaji wa Afrika wa klabu ya FC Rostov wanataka kocha Gamula atimuliwe

    (GMT+08:00) 2014-11-04 10:35:57

    Wachezaji kutoka Afrika waliopo kwenye klabu ya FC Rostov wanataka kocha Igor Gamula afukuzwe kazi kwa madai ya kutoa maoni ya kibaguzi. Maoni hayo aliyatoa baada ya kuulizwa kama atamsaini mchezaji wa Cameroon, ambapo Gamula aliwajibu waandishi wa habari kuwa klabu yake inawachezaji wa kutosha weusi, na wana sita kati ya watu hao. Matokeo yake wachezaji akiwemo kutoka Afrika kusini Siyanda Xulu wanataka afukuzwe. Akijitetea Gamula amesema hajawahi kuwagawa wachezaji kwamba kuna wazuri au wabaya, wageni au warussia, na pia aliiomba radhi timu. Xulu ni mmoja wa wachezaji katika kikosi, pamoja na wenziwe kutoka Angola, Mali, Gabon na Ivory Coast. Gamula amesema wachezaji wote walifanya mazoezi jana Jumatatu na kuongeza kuwa alikuwa na wasiwasi mkubwa na hakulala kwa siku mbili kwani hakutaka kumtukana au kumkasirisha yeyote yule. Rostov ni mmoja ya miji itakayokuwa wenyeji wa kombe la dunia mwaka 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako