Mratibu wa kimataifa wa Ebola kupitia Mfuko wa kuhudumia watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) Peter Salama amesema, shirika hilo litaongeza maradufu wafanyakazi wake katika nchi za Guinea, Liberia, na Sierra Leone ambazo zimeathiriwa zaidi na Ebola. Amesema watoto wanachukua asilimia 20 ya watu wenye maambukizi ya Ebola katika nchi hizo, na kwamba karibu watoto milioni 5 wameathirika na ugonjwa huo, huku watoto wengine 4,000 wakiachwa yatima.
Amesema ugonjwa huo umesababisha kufungwa kwa shule, watoto kufungiwa majumbani na kutoruhusiwa kucheza na watoto wengine kutokana na hofu ya maambukizi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |