Waendesha mashtaka wa Afrika Kusini wanataka ruhusa ya kukata rufaa dhidi ya mwanariadha Oscar Pistorius kwa kupewa hukumu nyepesi. Mwezi uliopita Pistorius alianza kutumikia kifungo cha miaka mitano jela kwa kumuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp, ingawa anaweza kutoka ndani ya miezi 10 tu. Waendesha hao mashtaka pia wamesema hukumu imeshindwa kuzingatia mauaji ya kutisha yaliyomkumba Steenkamp, lakini mbali na hayo pia watakata rufaa dhidi ya Pistorius kwa kutoshtakiwa kwa kuuwa kwa makusudi. Mawakili hao wamesema hukumu hiyo ilikuwa nyepesi sana na isingetolewa na mahakama yoyote ile inayotumia busara. Mawakili hao wanataka ahukumiwe miaka 15 jela. Pistorius hivi sasa anatumikia kifungo chake katika jela ya Kgosi Mampuru II katika kitengo cha hospitali, na anaweza kuomba kupewa kifungo cha nyumbani baada ya kukaa jela kwa miezi 10. Baada ya hukumu familia yake ilisema haitakata rufaa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |