Arsenal imekumbwa na kizaazaa kwenye ligi ya mabingwa hatua ya timu 16 bora baada ya kuchezea shilingi na kuidondosha chooni walipokuwa wakiongoza kwa mabao 3-0 dhidi ya Anderlecht. Bao la kwanza la Gunners lilingizwa na Mikel Arteta ambalo lilipatikana kwa njia ya penalti baada ya Danny Welbeck kufanyiwa madhambi na Chancel Mbemba katika dakika ya 25 kipindi cha kwanza. Na muda fupi tu Alexis Sanchez akazidi kuing'arisha Arsenal kwa kuongeza bao safi kabisa la pili alilolifunga akiwa umbali wa yadi 20, kabla ya Alex Oxlade kuingiza la tatu katika kipindi cha pili. Arsenal walikuwa tayari wameshajihakikishia kuwa wanaingia hatua ya mtoano lakini matumaini hayo yalizimwa baada ya kunyeshewa mvua ya magoli na wapinzani wao ambao walilipiza mabao yote matatu huku Gunners wakibaki kinywa wazi kwa mshangao. Bosi wa Gunners alionekana mwenye hasira mwisho wa mchezo. Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa matokeo yalikuwa sare ya mabao 3-3.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |