Winga Nani amesema hafikirii kabisa kurudi Manchester United. Mchezaji huyo alikwenda Sporting Lisbon kwa mkopo na kamwe haoni dalili ya kurudi kwenye kikosi chake. Ni wazi kuwa kocha mpya wa Man United Louis van Gaal wala hamfuatilii sana hivyo Nani mwenye miaka 27 ameibuka na kusema hana mpango na klabu hiyo. Gazeti moja la Ureno la O Jogo lilimkariri akitamka: kuwa wala hana mpango wa kurudi kwenye kikosi cha Man United, kwani anawapenda watu wanaompenda, na anaamini watu wanaomuamini kuwa ana uwezo wa kufanya vizuri. Amesisitiza kuwa akiwa huko Sporting Lisbon kila anapoamka anajiona mwenye nguvu zaidi, pia kuna viongozi wanaofahamu kuwa ana uwezo mkubwa na wanataka aonyeshe kiwango zaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |