Ofisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Silas Mwakibinga ameondolewa kwenye wadhifa wake huo. Kuondolewa kwa Mwakibinga kumekuwa kunahusishwa na sakata la mwanasheria Damas Ndumbaro dhidi ya uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Mwakibinga alikiri kuondoka akisema ni kweli hayupo kazini tangu Oktoba 31, ameamua kupumzika afanye mambo yake. Pia amesema TFF wanatakiwa washikane uchawi wenyewe kwani yeye hajawahi kuvujisha siri za bodi wala kutoa nyaraka zozote kinyume na taratibu, kwa nyaraka zinazosemwa hizo za mkataba wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), TFF wanatakiwa wamtafute mwanasheria wa TBL, wajitathmini. amesisitiza kuwa Ndumbaro yupo kwanini asiulizwe hizo nyaraka kazipata wapi? Kwa kuwa mkataba ni siri, sasa kama ni siri yeye kazipataje kama siyo kapewa na watu wa TFF au TBL. Nafasi yake imekaimiwa na makamu mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto. Taarifa ya TFF iliyotolewa juzi na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mashindano, Boniface Wambura ilieleza kuwa Mwakibinga amemaliza mkataba wake na kwamba wanamtakia heri katika majukumu yake mapya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |