• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanasoka wa zamani wa kimataifa wa Brazil ashitakiwa kwa kuwa na uhusiano na wauza dawa za kulevya

    (GMT+08:00) 2014-11-06 14:33:20

    Mwanasoka wa zamani wa kimataifa wa Brazil Adriano Leite Ribiero ameshitakiwa kwa kuwa na uhusiano na wauza dawa za kulevya mjini Rio de Janeiro. Mwendesha mashtaka alisema mchezaji huyo alimpatia pikipiki muuza dawa za kulevya ambaye ameitumia kwenye matukio ya uhalifu. Adriano mwenye miaka 32 yupo kwenye majadiliano na timu ya daraja la pili ya Le Havre ya Ufaransa. Tuhuma hizo ziliibuliwa mapema mwaka 2010 huku polisi nchini Brazil wakisema Adriano alinunua hiyo pikipiki mwaka 2008 na kuisajili kwa jina la mama wa muuza dawa huyo Paulo Rogerio de Souza Paz anayejulikana kwa jina maarufu la Mica. Pikipiki hiyo imekuwa ikitumika kusafirisha mihadarati katika vitongoji vya jiji la Rio na ikimilikiwa na genge maarufu la wahalifu la Commando Vermelho(Red Command).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako