• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ndoa iliyojaa mahaba kati ya mchina na mwafrika

    (GMT+08:00) 2014-11-06 17:04:56

    Ni safari ya maisha aliyokuwa akiyataka tokea utotoni. Akiwa amembega mwanae Emannuela wa miezi 10, Edwin Ata Rasiliamali kutoka Tanzania anaonekana mwenye furaha mpwito mpwito . Katika nyumba yake mjini Beijing, Edwin na mke wake mchina wanakumbuka jinsi walivokutana na kupendana mara ya kwanza wakiwa chuoni. Kwa Edwin, mapenzi hayachagui rangi wala dini.

    " Maisha yangu yote ya ujana nimekulia China. Kwanza kabisa nilikuja China mwaka wa 2005 kusomea shahada ya kwanza kabla ya kurudi Tanzania kufanya kazi na shirika la Star Times. Baadaye niliamua kuja tena China kwa shahada ya pili, hivyo ule ukaribu wangu na wachina, utamaduni na mapenzi nikaamua kuoa mchina. Tulioana mwaka jana mwezi wa sita" anakumbuka Bw Ata Rasiliamali.

    Mtoto wa Edwin na Chen Sisi. Ana umbo la nusu mwafrika na nusu mchina

    Mke wake Edwin. Sasa anaweza kupika baadhi vyakula vya kiafrika na atarajia kwenda Tanzania siku moja.

    Marafiki wa China wajiunga na Edwin na Mkewe Chen Sisi katika harusi yao kwenye ubalozi wa Tanzania nchini China.

    Edwin na mkewe Chen Sisi kwenye sherehe yao ya harusi iliofanyika katika ubalozi wa Tanzania nchini China. Edwin alikuja China mwaka wa 2005 kusoma.

    Edwin Kutoka Tanzania akiwa na mtoto wake Emmanuela mwenye umri wa miezi 10.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako