• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Manchester City yagaragazwa nyumbani na CSKA Moscow

    (GMT+08:00) 2014-11-07 10:07:20

    Safari ya Manchester City kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani Ulaya imeingia dosari baada usiku wa kuamkia jana kukubali kipigo nyumbani Etihad na Warusi wa CSKA Moscow na kuufanya kuwa usiku mbaya jijini Manchester. Licha ya kuruhusu mabao mawili ya kipindi cha kwanza yaliyotiwa wavuni na Seydou Doumbia pia viungo wake muhimu Yaya Toure na Fernandinho walitolewa nje kwa kadi nyekundu na hivyo wataikosa mechi ngumu ijayo dhidi ya Bayern Munich. Yaya Toure alisawazisha bao la kwanza la Doumbia lakini haikusaidia kitu kwani mchezo wa chini ya kiwango unaoikabili timu hiyo hivi karibuni umeigharimu katika kundi lake kiasi cha kucheza mechi nne na kupata pointi mbili tu. City haijashinda hata mechi moja na sasa wanapaswa kuzifunga Munich na Roma katika michezo iliyosalia ili kupata njia ya kusonga mbele hatua ya 16 bora. Yaya Toure amewaomba radhi mashabiki na wapenzi wa timu yake kwa kupewa kadi nyekundu kwa mara ya kwanza akiichezea Man City. Mechi zinazofuata zitachezwa Novemba 25.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako